Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) amesema jografia ya Tanzania ina fursa kubwa ya kufanya biashara ya mazao kilimo na nchi takriban saba.
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo wakati wa majumuisho bada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya biashara ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika jijini Mbeya.
Waziri Mkuu Majaliwa amesema sera za kilimo nchini Tanzania zimebadilika na kuwa na mwelekeo wa kibiashara, hivyo ni wakati wa wanachi hususan vijana kuitumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kuchangia uchumi wa Taifa.
Waziri Mkuu Majaliwa ameongeza kuwa hatua ya Serikali kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo hadi kufikia bilioni 900 ina lengo la kuwezesha idadi kubwa ya wananchi kujikwamua kiuchumi.
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kuridhishwa kwake na maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane kwa mwaka huu 2023, kwani ameona maboresho makubwa ikilinganiswa na yake yaliyofanyika mwaka jana.