Wakulima na Wafanyabiashara wa mazao ya kilimo wameshauriwa kurasimisha biashara zao ili kunufaika na fursa za uuzaji na ununuzi wa mazao yao kwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Ushauri huo umetolewa na Mchumi wa Wizara ya Kilimo, Maria Mtui katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mtui amezitaja faida kadhaa za urasimishaji wa biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalinda wakulima na wafanyabiashara dhidi ya usumbufu na utapeli unaotokea kwenye biashara ya mazao.
Aidha Mtui amebainisha kuwa wakulima wa hapa nchini wataendelea kunufaika na jitihada za serikali za kutoa huduma kadhaa ikiwemo ruzuku mbolea kwa wakulima na ili kupunguzia gharama za uzalishaji.