Awamu ya kwanza ya Mafunzo ya kutengeneza vihenge vya chuma kwa vijana (artisan) yanayotelewa na mradi wa TANIPAC kwa kushirikiana na Taasisi ya Ufundi Sanifu (VETA) yameanza katika vituo mbalimbali nchini. Awaamu ya kwanza imechukua vijana ... katika vyuo vya Morogoro, Dodoma, Manyara, Tabora, Mwanza, na Kigoma. Mafunzo haya ya wiki mbili yatawawezesha vijana kutengeneza vihenge vya chuma kwa ajili ya kuhifadhi mahindi na karanga katika juhudi za kudhibiti tatizo la sumukuvu katika nafaka.