Mafunzo ya udhibiti wa Sumukuvu kwa kutumia kanuni bora za Kilimo na matumizi ya Aflasafe

Mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwa wakulima yanayoendelea katika Halmashauri 18 za Tanzania Bara zinazotekeleza mradi yamefika katika Halmashauri ya Buchosa ambapo jumla ya wakulima 3,000 katika Halmashauri hiyo watafikiwa. Katika picha, mtaalam Jonathan Sylvester kutoka Wizara ya Kilimo akiwa anakazia jambo wakati wa mafunzo hayo kwa wakulima viongozi waliochaguliwa ambao nao watawajibika kuwafundisha wakulima wengine 10 (kila mmoja) chini ya usimamizi wa Afisa Kiungo wa Mradi na Mabwana shamba wa maeneo husika.